Mkuu (SMAUJATA) Idara ya Wanafunzi Vyuo na Vyuo Vikuu Taifa Irene Robert Mashine amewataka wanafunzi wa Vyuo kutoa fumbia macho vitendo vya ukatili wa ikiwemo usafirishaji haramu wa binadamu, kingono wawapo vyuoni.
Irene ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo kikuu cha TUMAINI (TUDARCO) katika semina iliyolega kutoa elimu kwa kundi hilo namna ya kupambana na changamoto hizo hasa biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Amesema kwenye vyuo vingi wanafunzi wamekua wakifanyiwa ukatili lakini wamekua wakinyamaza na kushindwa kuzungumaza kwa watu jambo ambalo lina waathiri kisaikolojia katika masomo.
Anasema wengine wamekua wakiombwa rushwa ikiwemo ya ngono na pesa jambo hilo halipaswi kuzoeleka wala kufumbiwa macho kwani linaharibu dhima ya utu wao.
Aidha Irene amewataka wanachuo kutambua nafasi zao,kwanini wapo chuo,wanamalengo gani,watimize majukumu yao pamoja na kufuata na kuachana na tamaduni za watu wengine ambazo zipo nje ya utu na utamaduni wa kitanzania,
Aidha Mkuu wa idara bi Irene Mashine alimshukuru Mh Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuliona hili na kuagiza yaundwe madawati ya jinsia vyuoni,na kumpongeza Mh
Dorothy Gwajima waziri mwenye thamana kwa kulifanyia kazi,naye ameahidi Kama mkuu wa idara akishirikiana na wanasmaujata Tanzania nzima .