Ni Kijana wa kitanzania Makoye Philbert maarufu kama MakJuice ambae jina lake lilitikisa jiji la Dar es Salaam kwa uuzaji wa Juice na kisha kupewa nyota tano mabegani na wadau mbalimbali kutokana na ubunifu wenye viwango vyote.
Mbali na kwamba stori yake iliwagusa wengi ya kuanza na mtaji wa Shilingi Elfu za kitanzania kwenye uuzaji wa biashara ya Juice, sasa leo hii June 23, 2023 Makoye anazungumza na Milllardayo.com & Ayo TV akieleza sababu za kuisimamia biashara yake ya pili aliyoipa jina la Makchicken kwa muda wa miaka 3 kisha kuirejesha tena.
‘Maneno yalikuwa mengi mitandaoni lakini sikukata tamaa na yapo yaliyokuwa yakisemwa juu ya biashara yangu lakini unajua katika Safari wapo watakakubali kile unachofanya na wapo ambao watapinga ndio Challenge ya maisha lakini sikuvunjika moyo kwani naangalia mbele nina Focus na kile ninachokifanya’- Mkurugenzi wa Makjuice & Makchicken, Makoye Philbert
‘Yaliongelewa mengine sana kuhusu biashara hii lakini ukweli ni kwamba mimi nilisimama kutokana na Serikali ilikuwa kwenye kuboresha miundombinu yaani ujenzi wa Barabara hivyo nikaona nisimamie kwa muda mpaka muda utakaosahihi wa mimi kufikiria eneo husika wa hii biashara kwani ilikuwa ni jambo la Ghafla sana’– Mkurugenzi wa Makjuice & Makchicken, Makoye Philbert
‘Basi ilinichukua kama miaka mitatu kukaa na kuwaza nileta ama nifanye nini kilichobora bor, basi nikapata wazo la kwamba katika kuadhimisha miaka 7 ya Makjuice lazima uendane na mabadiliko kwahiy0 ilinibidi niboreshe eneo husika la linahusika na kuuza juice kisha ambapo awali tulianza na Kibanda kisha tukafuata Kontena lakini leo hii nikapafanya pakawa kama mgahawa ambao wateja wetu wanaofika waweza pata mahala pakukaa na kunywa ama kuhudumiwa kwa kile wanachokihitaji’- Mkurugenzi wa Makjuice & Makchicken, Makoye Philbert
‘Kutokana na mapinduzi hayo ya maboresho ndipo sasa nikaamua kuirejesha tena Makchicken ambapo safari hii kuku wana Viwango wa hali ya juu, nimeweka viungo ambavyo ladha wa kuku wa awamu ya kwanza ni tofauti na awamu hii ya pili kwani Kuku wetu tunatengeneza kwa kutumia viungo vya asili vya hapa hapa Tanzania na wala si popote’- Mkurugenzi wa Makjuice & Makchicken, Makoye Philbert
‘Ofisi zetu ziko pale pale Sinza Afrika Sana mkabala na Sheli ya State Oil na katika kutekeleza jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mimi kama Kijana nimeona niungane na Serikali katika suala la kutoa ajira na ukifika ofisini basi utapokelewa na kuhudumiwa na vijana mahiri wenye kusikiliza wateja kwa kila unachohitaji kutoka kwetu’- Mkurugenzi wa Makjuice & Makchicken, Makoye Philbert
‘Ofisini kwetu zinapatikana Juice tofauti tofauti zote pia kwa wale wenye kuhitaji kupunguza uzito wa Mwili basi tuna Juice inaitwa GREEN FAT BUNER utaitumia mara mbili tu kwa siku Asubuhi na Usiku na ndani ya siku chache sana utakuwa umepunguza kilo za kutosha, inapatikana Makjuice kwa oda na kuanzia LITA MOJA, Tupigie 0747111172 kwaajili yakuweka oda na kufanyiwa Free Delivery kwa waliopo kwenye jiji hili la Chalamila DSM’- Mkurugenzi wa Makjuice & Makchicken, Makoye Philbert
“Karibuni tuwahudumie Ofisini zetu ziko wazi kuanzia Jumatatu Mpaka Jumapili na saa za kazi ni kuanzia Asubuhi saa nne asubuhi mpaka saa tano kamili Usiku’– Mkurugenzi wa Makjuice & Makchicken, Makoye Philbert