Wananchi wa kata ya daraja mbili jijini Arusha wamefanya Maandamano ya hiari kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kupinga na kutokomeza matumizi ya Dawa za Kulevya nchini na kuitaka serikali kuongeza mkazo katika kudhibiti uingizaji ,na Ulimaji wa Madawa hayo.
Akiongea na Wananchi baada ya maandamano hayo, afisa Mtendaji wa kata hiyo Joseph John alisema wimbi la matumizi ya dawa hizo katika kata hiyo ni kubwa na linalosababisha athiri kubwa wa vijana wakiwemo wanafunzi wa Shule na vyuo.
Alisema kata hiyo ambayo ni miongoni mwa Kata 25 za jiji la Arusha imejipanga vema kumuunga mkono Rais Samia ambaye ni mgeni rasmi Siku ya Maadhimisho ya Dawa za Kulevya kitaifa yanayofanyika Mkoani Arusha kuhakikisha biashara hiyo inatokomezwa ikiwemo kufanya msako wa nyumba kwa nyumba.
Alisema asilimia 90 ya vijana katika kata hiyo ya Daraja mbili wamekosa sifa za kupatiwa mikopo kutokana na wengi wao kuathiriwa na matumizi ya dawa hizo na hivyo hadi sasa hakuna kikundi hata kimoja cha vijana walionufaika na mkopo usio riba kutoka halmashauri ya Jiji la Arusha.
Naye Askari Polisi Kata, Inspekta Festo Bulali alisema kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likitoa Elimu juu ya athari za Matumizi ya Dawa za Kulevya na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwabadilisha vijana wasijiingize kwenye Ulevi huo.
“Jeshi la polisi Kupitia kitengo la Polisi Jamii na kamisheni ya ushirikishwaji limejikita zaidi katika utoaji wa elimu ,wakazi wa daraja mbli wanahitaji elimu zaidi ya kupinga matumizo ya dawa za kulevya”
Naye mwenyekiti wa ccm kata ya daraja mbili ,Adam Maris alisema chama cha mapinduzi kimejipanga kuongea na wananchi nyumba kwa nyumba ili kuwaelimisha juu ya athairi za matumizi ya dawa za kulevya ,Uhalifu pamoja na matumizi ya Pombe haramu.