Mradi wa Ujenzi wa Reli yenye kiwango cha kimataifa(SGR), unaoendelea nchini Tanzania umekuwa kivutio kwa Nchi mbalimbali barani Afrika zilizoshiriki katika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyofanyika Victoria Falls, Zimbabwe kwa mara ya tisa tangu kuasisiwa, Maonesho yameanza tarehe 21 Juni hadi 23, 2023.
Shirika la Reli Tanzania(TRC) ni miongoni mwa Taasisi ya Serikali iliyofanikisha ushiriki katika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika, Maonesho haya yamebeba dhima chini ya kauli mbiu kuu isemayo ”Eneo Huru la Biashara katika Bara la Afrika litahitaji Utawala wa Umma wenye nia madhubuti ili kufanikiwa”
Wataalamu wa mambo ya usafirishaji duniani wanasema usafiri wa reli hupunguza gharama ya bidhaa kwa asilimia kati 30% hadi 40% na huwa nikichocheo kikubwa cha uchumi,kuwekeza katika ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa Tanzania.
Muwakilishi Mkuu katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa umma barani Afrika kutoka Tanzania ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti na utawala bora Ridhiwani Jakaya Kikweta,alipata fursa ya kuchangia katika kikao cha maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma barani Afrika kipindi cha majadiliano kuhusu maendeleo ya biashara huru kwa nchi za Afrika lakini pia alielezea uboreshaji wa miundombinu, ikiwemo reli, barabara majengo pamoja na kuhakikisha utumishi wa umma unakua bora na wenye tija ili kufikisha malengo katika bara la Afrika.