Katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) Kampuni ya TanzaKwanza ikishirikiana na TANTRADE imeandaa mabanda maalumu yatakayowezesha ushiriki wa kipekee wa sekta mbali mbali za uchumi.
Mabanda haya yenye hadhi ya kimataifa na yatakayokuwa na Teknolojia ya kisasa yatahusisha Sekta za Madini, Tehama, Mazingira, Misitu na Ufugaji wa Nyuki, pamoja na Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Malengo ya TanzaKwanza katika kuandaa mabanda haya maalumu ni
1.Kukuza na kuuza bidhaa, huduma, na wataalamu wa Tanzania 2.Kushirikisha wadau katika midahalo ya kisekta
3.Kutambua vinara wa kisekta ambao wamekuwa wakitoa
bidhaa na huduma zenye ubora wa kimataifa.
Makampuni na mashirika yatakayokuwa chini ya usimamizi wa mabanda haya watapata nafasi ya kipekee ya kukutanishwa na wawekezaji kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo China, Ujerumani, Japan, India, Umoja wa Falme
Wawekezaji hawa wanakuja kwa mualiko maalumu wa TanzaKwanza na watakutanishwa na wafanyabiashara wa sekta zilizotajwa kupitia mikutano maalumu itakayoandaliwa na TanzaKwanza.
Tunakaribisha wadhamini kutoka ndani na nje ya nchi ili kufanikisha maandalizi ya mabanda haya. Wadhamini watapata nafasi za kipekee za kuweka chapa katika mabanda haya na kuongoza mada za midahalo ya kisekta.
Tanzakwanza ni kampuni ya kiasasa ya Masoko inayotumia mikakati madhubuti na teknolojia ya kisasa katika kufikia wateja ndani na nje ya nchi. Kupitia wataalamu waliobobea katika sekta hii, kampuni hii inaongoza kwa ubunifu na imesaidia wateja kuunda Chapa zisizosahaulika.