Mbunge wa jimbo la Ulanga na Mkurugenzi wa kampuni ya Ruby International Limited Mheshimiwa Salim Alaudin Hasham ameahidi kutoa kiasi cha Shilingi Milioni nne kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya Ladies Talk Tanzania Initiative .
Mheshimiwa Salim ametoa ahadi hiyo wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Wanawake za fani mbalimbali zilizoandaliwa na taasisi hiyo iliyofanyika mjini Morogoro.
Mheshimiwa Salim amesema ameamua kutoa msaada kwa taasisi hiyo kutokana na kazi kubwa wanayofanya kuhamasisha wanawake kujitegemea katika shughuli za kimaendeleo na kuepukana na kua tegemezi kwa kufanya kazi za ujasiriamali.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye ndiye mgeni rasmi ameahidi kutoa Shilingi milioni tano na laki tatu kwa taasisi ikiwa ni mwendelezo wa kuunga mkono juhudi za taasisi.
Mhe. Naibu waziri amesema wanawake wanatakiwa kubadilika kuacha kua tegemezi badala yake wajitume katika utafutaji wa fedha
Amesema kupitia simu za mkononi wanaweza kujifunza mambo mengi ya ujasiriamali na kupata wateja.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Ladies Talk Tanzania Salome Sengo amesema Taasisi hiyo imejikita kutoa elimu ya ujasiriamali,kupinga vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto pamoja na kuhamisha wasichana kupenda elimu.