Ni June 25, 2023 ambapo MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham ametoa kauli kwa Wananchi kufuatia kukatika kwa daraja linalounganisha kata ya Mwaya na Mbuga.
Akizungumza na Millardayo.com Mhe Salim Alaudin Hasham amesema…’Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kukatika kwa daraja muhimu linalounganisha kata ya Mwaya na Mbuga, Natoa pole kwa wananchi waliopata madhara pia niwape pole wananchi wote ambao watapata usumbufu kwa kipindi hiki kifupi, Mimi kama mwakilishi wenu kwa kushirikiana na mamlaka husika tunalishughulikia kwa haraka kutatua tatizo hilo ili shughuli za kiuchumi na kibinadamu ziweze kuendelea’- Mhe Salim Alaudin Hasham Mbunge wa Jimbo la Ulanga