Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu aliwatembelea wanajeshi wa Urusi walioshiriki katika operesheni ya kijeshi nchini Ukraine, shirika la habari la RIA Novosti limeripoti, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuonekana hadharani tangu maasi ya wikendi ya kundi la wanamgambo la Wagner.
Ripoti ya RIA, iliyoitaja wizara ya ulinzi ya Urusi, iliweka wazi Shoigu alisalia madarakani, lakini haikutoa maelezo kuhusu ni lini au wapi alikutana na wanajeshi na makamanda wa wilaya ya kijeshi ya Magharibi.
Waasi hao wakiongozwa na mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin walisonga mbele kwa Moscow ili kuondoa kile walichokiita uongozi wa kijeshi fisadi na usio na uwezo wa Urusi, kabla ya kurejea ghafla katika eneo linaloshikiliwa na Urusi mashariki mwa Ukraine baada ya makubaliano na Ikulu ya Kremlin iliyosimamiwa na kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko.
Makubaliano hayo yalijumuisha kinga kwa waasi badala ya kurejea kambini, lakini bado haijafahamika iwapo Putin pia alikubali kufanya mabadiliko ya uongozi wa juu wa kijeshi au kufanya makubaliano yoyote mengine.
Katika video iliyotolewa Jumatatu asubuhi na Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Shoigu alionyeshwa akiruka ndani ya ndege na mfanyakazi mwenzake na kusikia ripoti katika kituo cha amri kilichoendeshwa na kikundi cha kijeshi cha Zapad (Magharibi) cha Urusi.
Hakukuwa na sauti kwenye video hiyo na haikufahamika mara moja ni wapi au lini ziara hiyo ilifanyika.
Kanali ya Televisheni ya Wizara ya Ulinzi ya Zvezda ya Russia imesema Shoigu, ambaye alionekana kutojeruhiwa kimwili na mtulivu, amesikiliza ripoti ya Kanali Jenerali Yevgeny Nikiforov, kamanda wa kundi hilo kuhusu hali ya sasa kwenye mstari wa mbele nchini Ukraine.