Drake ametangaza albamu yake mpya inayoitwa For All The Dogs pamoja na kuachia kitabu chake cha mashairi cha Titles Ruin Everything.
Mashabiki waliona [msimbo wa QR] QR code katika matangazo kadhaa ya magazeti siku ya Jumamosi ikiwa ni pamoja na New York Times. Mashabiki walipotumia code hiyo, iliwaongoza kwenye tovuti titlesruineverything.com ambapo walipata ujumbe direct kutoka kwa Drizzy mwenyewe.
“Sijui kama nimewahi kutaka watu wanunue au kuunga mkono kitu zaidi katika maisha yangu…kitabu chetu cha kwanza kinapatikana tmrw kwenye @drakerelated na wauzaji wengine waliochaguliwa,” Drake aliandika wakati akitangaza kitabu hicho jana.
“I don’t know if I have ever wanted people to buy or support something more in my life…our first book is available tmrw on @drakerelated and other select retailers,”
“Nilitengeneza albam ya kwenda na kitabu… Wanasema wamemiss Drake wa zamani girl msinijaribu,”
“I made an album to go with the book… They say they miss the old Drake girl don’t tempt me,”
Tarehe ya kutolewa kwa albamu bado haijajulikana lakini tunakisia kuwa itafika wakati wa ziara yake ya It’s All A Blur itaanza Juni 29 huko Memphis, TN. Pia anaonekana kwenye nyimbo mbili kwenye albamu mpya ya Young Thug Business is Business.