Katika kuendelea kumuenzi Mwl.Julius Kambarage Nyerere Chuo kikuu cha dar es salaam kimefanya Tamasha la 14 la “Mwalimu JK Nyerere Intellectual festival “ (tamasha la kisomi la taaluma la nyerere) ili kuyaenzi maono ya rais wa kwanza wa Tanzania katika kutatua matatizo yanayoikumba afrika ikiwemo kujenga azma ya demokrasia, usalama na maendeleo ndani ya Afrika.
Prof. Rwekaza Mukandala profesa wa kigoda cha mwalimu Nyerere cha kitaaluma cha wanajumimuiya wa Afrika kutoka chuo kikuu cha dar es salaam (UDSM) amesema wameendelea kufanya tamasha hilo kwa Mara ya kumi na nne sasa na kualika wasomi na wanataaluma maarufu ambao wanaelezea masuala muhimu katika bara la Afrika ambapo kwa mwaka huu wamemualika mwanataaluma kutoka nchini Kenya.
Kwa upande wake profesa Muhadiri chuo kikuu cha Nairobi Prof. Musambayi Katumanga amesema waendelea kumuenzi mwl.Nyerere kwa kutumia njia alizotumia na mambo aliyoanza kuyatatua na kwamba vita vya afrika vinatoka na watu wanavyotaka kugawana mali na rasilimali huku serikali zikiwa hazitiloa maanani kwa kushindwa kuwaweka watu wao pamoja.
Zaidi ya robo ya nchi za afrika zina vita za wenyewe kwa wenyewe na pia nchi nyingi Zina ongozwa na viongozi wale wale kwa miaka mingi tatizo la utawala bora usalama na umoja wa afrika yamekua yakirudi nyuma hivyo, jukumu la waafrika ni kuhamasika kuelewa kwa undani mambo yanatoendelea ili kuweza kujikomboa kiuchumi .
Kwa upande wake muwakilishi wa haki elimu Richard mabala mwenyekiti wa bodi ya haki elimu amesema haki elimu inaunga mkono tamasha hili kwa kukwa linaendana na malengo ya haki elimu katika kupanua mawazo na kujenga jamii yenye haki na usawa na tamasha linapanua magazine ya wanajamii, dhamira kuu ni kujenga kidemocrasia.
Kwa upande wake profesa muhadiri chuo kikuu cha Nairobi musambayi katumanga amesema waendelea kumuenzi mwl.nyerere kwa kutumia njia alizotumia na mambo aliyoanza kuyatatua na kwamba vita vya afrika vinatoka na watu wanavyotaka kugawana mali na rasilimali huku serikali zikiwa hazitilii maanani kwa kushindwa kuwaweka watu wao pamoja