Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba leo Bungeni Dodoma amewataka Watanzania kutohofia kuongezeka kwa ushuru wa barabara na mafuta kwa kiasi cha shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta ya petroli na dizeli.
“Serikali inafanya ufuatiliaji wa ndani kuhusu soko la dunia kwenye masuala ya nishati ya mafuta, tena Watanzania msiwe na hofu na hii Tsh 100 kwenye mafuta kwa sababu kuna wakati mafuta yalipanda kwenye soko la dunia sio hata kwa ajili ya sh 100 Serikali ikaweka ruzuku, hili ni jambo jema kwa maana linataka kutunisha mifuko ya Serikali katika kutekeleza miradi ya Serikali” —— Dr. Mwigulu