Mkahawa mmoja wa rameni[tambi] huko Yunlin, Taiwan, ulizindua menyu yake ya hivi punde – ya Godzilla Ramen, bakuli la supu ya rameni na mguu wa mamba uliopambwa ndani ya supu taamu ndani yake.
Rameni ya Taiwan imekuwa ya kushangaza zaidi katika wiki chache zilizopita kwani kipo chakula kingine ambacho chenyewe huitwa ‘Frog Frog Ramen’ yani tambia za vyura .
Inasemekana kwamba sahani hiyo imetengenezwa kwa viungo 40 tofauti, lakini kiungo kikuu kinachotoka kwenye bakuli ni mguu wa mamba uliotengenezw kitaalamu zaidi
Nu Wu Mao Kuei alitangaza kwenye Facebook kuzindua tambi hizo za mamba “Godzilla”, ambayo hutayarishwa kwa kuanika au kunyoosha mguu wa mbele wa mamba na katika clip hiyo yupo mteja anaelezea kuhusu ladha ya chakula hicho na kuelezea mlo huo kuwa wa kupendeza.
Na anasema ladha inafanana na kuku, au ladha sawa na miguu ya nguruwe. SETN iliripoti.
.