Timu mpira wa miguu Mashujaa FC imepokelewa mkoani kigoma na mashabiki wa soka baada ya kutoka Mbeya kwenye mchezo wake wa mkondo wa pili ya kuwania tiketi ya kutinga Ligi kuu Tanzania bara mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa sokoine ikiwa ni Mbeya City 0 – 1 Mashujaa Fc.
Timu hii imelakiwa kutoka Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma hadi katika Viwanja vya mwanga manispaa ya Kigoma Ujiji na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh.Thobias Andengenye.