Katika habari zilizo kamata headline wiki hii bi story ya mwanamume mmoja huko Georgia mwenye umri wa miaka 27 hivi majuzi alitumia $81,000 zaidi ya mill 197 kwaajili upasuaji wa kuongeza mguu baada ya kukataliwa na mpenzi wake, ambaye alimwambia kuwa alikuwa mfupi sana.
Mwanaume huyo ametambuliwa kama daktari wa zamani wa Jeshi la Wanamaji anayeitwa Dynzell Sigers, na baada ya kukataliwa na crush wake ndipo alipoamua kufanya utaratibu wa kurefusha mguu, sasa anadai kwamba anahisi “kama mtu mpya.ambao ulimsaidia kuwa na urefu wa futi moja.
Katika mahojiano ya hivi majuzi, Sigers alifichua ni kiasi gani alitumia kukuza urefu wake kutoka futi 5 inchi 5 hadi futi 6 kwa urefu. Alisema, “Siku zote nilikuwa mtoto mwenye haya na mwenye kujizuia na siku zote niliogopa kuwa mimi mwenyewe kwa kuogopa kuhukumiwa au kutokubaliwa.
‘Na katika ujana wangu, siku moja nilikataliwa na msichana niliyempenda sana na ingawa aliniona kuwa mwenye kuvutia, mawazo yake yalikuwa kwamba nilikuwa mfupi sana na mdogo sana kwake.”
Sigers aliendelea kueleza jinsi kukataliwa na mwanamke huyo, hasa juu ya ufupi wake, kulivyomsumbua sana na anasema alikuwa amechoka na wanawake kumwambia kwamba yeye ni mfupi sana, kwamba hatimaye ilifanya uchumba uwe mgumu zaidi kwake.
Alieleza, “Jambo jingine kubwa ambalo lilinivutia ni kwamba kwa jinsi nilivyopenda kucheza michezo na nilikuwa mzuri sana, nilikataa kujiunga na timu yoyote ya shule yangu kwa sababu ya ufupi wangu.”
Kwa miaka mingi, Sigers amejaribu kutafiti taratibu na mbinu za jinsi ya kuongeza urefu wake ndipo kisha akajipata kwenye page inayohusu masuala ya upasuaji wa kuongeza mguu, na mara moja akapiga simu na kujiandikisha ili kufanyiw aupasuaji huo.
Alisema kuwa ilichukua upasuaji sita tofauti, ambao alianza Desemba 2022.