#GUMZO-Mama mmoja huko Ohio ameshtakiwa kwa mauaji baada ya kumwacha mtoto wake wa miezi 16 nyumbani kwa wiki moja alipokuwa likizo huko Puerto Rico na Detroit.
Kristel Candelario wa Cleveland, alimwacha mtoto wake nyumbani peke yake bila uangalizi wowowte kuanzia Juni 8 hadi Juni 16 na mwanamke huyo aliyetambiliwa kama Candelario aliporudi alimkuta binti yake, Jailyn, amefariki.
Polisi wanasema Kristel Candelario, 31, alikiri kumwacha msichana wake, Jailyn, nyumbani kwao Cleveland peke yake kwa siku nane, “akiwa peke yake na bila kushughulikiwa kwa chochote ikiwemo chakula, maji au usafi.”
Mwili wa mtoto huyo ulidaiwa kuwa katika hali ya kutatanisha, mamlaka iliongeza.
Candelario alifikishwa mahakamani kujibu mashtaka Jumanne asubuhi na kwa sasa anazuiliwa katika Gereza la Kaunti ya Cuyahoga kwa dhamana ya dola milioni moja, huku tarehe yake ijayo ya mahakama ikipangwa Juni 28 saa 8:30 asubuhi.