Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson asubuhi hii ya leo June 27,2023 ameahirisha shughuli za Bunge kwa muda baada ya kengele ya tahadhari kulia ndani ya ukumbi wa Bunge.
Dkt. Tulia ameahirisha shughuli hizo hadi hapo changamoto hiyo itakapopatiwa ufumbuzi ambapo amewataka Wabunge kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge haraka.
Kengele imelia wakati Wabunge wakiendelea na kipindi cha maswali na majibu.