Alex Klein, mjasiriamali wa teknolojia ambaye alifanya kazi na rapa huyo ambaye sasa anajulikana kama Ye jina mabalo alitumia kwenye albamu yake ya Donda 2 aliamua kusitisha ushirikiano baada ya tabia mbaya, ikiwa ni pamoja na kumsifu Hitler hadharani na alijikuta mwishowe akipokea maneno ya hasira, chuki ya ubaguzi wa rangi.
“Tulikataa dola milioni 10. Kanye alikasirika sana,” anasema Klein katika filamu ya BBC The Trouble with KanYe.
“Alikuwa akisema ‘Ninahisi kama nataka kukupiga’ na ‘wewe ni kama Wayahudi wengine’ na akitumia misemo hii akitumaini kuniumiza”.
“Nikamuuliza: ‘Je, unafikiri Wayahudi wanafanya kazi pamoja kukuzuia?’ na akasema ‘ndiyo, ndiyo .’
Kulingana na Klein, ambaye alifanya kazi na West kati ya 2019 na 2022, matamshi yake ya hadharani ya chuki ni mkakati wa kisiasa na wa makusudi.
“Anadhani ni hatima yake ya wazi, hatima yake mteule wa mungu kuwa rais. Alitumia kauli hizi za kupinga Uyahudi kama sehemu ya jukwaa la kisiasa na aliniambia kuwa alikuwa akijaribu kufanya kile Trump alifanya kwa njia kali zaidi.”
West, alikabiliwa na msukosuko mkubwa mnamo 2022 baada ya kutoa matamshi machafu kwenye Twitter na pia kushiriki nadharia za njama dhidi ya Wayahudi na kudai kwamba “amezuiliwa” na “vyombo vya habari vya Kiyahudi”.
Dili la rapa huyo wa “Touch the Sky” na Adidas kwa ajili ya brand yake ya viatu vya Yeezy lilivunjika mara baada ya kutoa maoni yake kwenye mitandao ya kijamii, ambayo inasemekana kumpoteza $1.6bn ya thamani yake siku zote.
Balenciaga pia alikata uhusiano na West, bila kusahau Vogue na Anna Wintour walisema kwamba hawakuwa na nia ya kufanya kazi na Kanye tena.