Mwigizaji wa Ghana, Yvonne Nelson amejibu kauli ya rapa aliyeshinda tuzo, Sarkodie kuhusu kuharibu mimba lakini kumbuka kwamba Yvonne katika kitabu chake alisema Sarkodie alimwacha baada ya kumpa ujauzito na mwishowe alisema uamuzi wa rapa huyo kutokubali kuwajibika kwa ujauzito wake ulimfanya atoe mimba hiyo.
Mwigizaji huyo alifichua hayo katika kumbukumbu yake, ‘I Am Not Yvonne Nelson’ iliyozinduliwa Jumapili, Juni 18, 2023.
Na madai yake dhidi ya Sarkodie yapo katika ukurasa wa 88 hadi 95 wa kitabu hicho, ambapo alidai rapper huyo alimpa ujauzito mwaka wa 2010, lakini akasema hapana kabisa kumtunza mtoto huyo ndiomaan akaitoa.
“Sikuwa mimi pekee niliyehusika na hali hiyo, kwa hivyo nilimwita mtu ambaye mbegu yake yenye nguvu ilikuwa imekuwa ndani yangu jina lake ni Michael Owusu Addo, mwanamuziki mashuhuri wa Ghana ambaye anajulikana zaidi kama Sarkodie,” alisema.
Lakini akijibu, katika wimbo wake mpya zaidi, ‘Try Me ‘ uliotolewa siku ya jana, Sarkodie alidai alimwomba Yvonne Nelson kubaki na ujauzito huo ingawa hakuwa tayari kuwa baba.
“Ndio, sikuwa tayari lakini nilikuambia uihifadhi. Kwa hivyo usifanye ionekane kama nilikuwa nakusukuma kutoa mimba,” moja kati ya ubeti wa kwanza kwenye wimbo huo.
“I’m not going to lie, we had a thing. First, I thought we had a think until I had the hint that there were many guys. I tried to stay away but then you came that you were pregnant. But then I wasn’t ready but I told you to keep it.
“You told be you were schooling so you needed to complete it but till today, I don’t believe it. I told you to let my doctor take care of you and you sent a text later that your friend has recommended a one of the best doctors…
Hata hivyo, siku ya Jumatano mwigizaji huyo alimhoji Sarkodie kwa kutumia rap ili kuyaondoa maumivu yake .
Aliandika kwenye Twitter, “Katika kitabu changu, nilisimulia jinsi ulivyonipa ujauzito, Jinsi ambavyo hukuweza kungoja niitoe. Jinsi Ulivyonifukuza ili kutoa mimba.