Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Ne-Yo, Sade Bagnerise amejibu ombi la hivi majuzi la mwimbaji huyo la kulea mtoto pamoja.
Siku ya Jumanne inasemekana mwanamke huyo alidai malezi ya msingi ya watoto wao wawili pamoja na matunzo ya kila mwezi ya mtoto pia alikubali kushiriki ulezi wa pamoja wa kisheria, ambao utamruhusu Ne-Yo kuwa na sauti katika masuala ya maisha ya watoto wao.
Katika taarifa za awali la Ne-Yo, pia aliomba kupimwa DNA ili kujua kama yeye ni baba wa mtoto wao na Bagnerise huku akikiri wa kwanza bila shaka ni wake. Katika majibu yake, hakushughulikia mahitaji lakini alibainisha, “[Ne-Yo] ni baba mzazi wa watoto hao.”
Maisha ya mapenzi ya Ne-Yo yamekuwa sio mazuri hivi karibuni na mnamo Februari, alikamilisha talaka yake kutoka kwa Crystal Renay, na akaishia kulazimika kuandika hundi ya karibu dola milioni 2 ili waachane.
Renay pia anachukua moja ya nyumba zao nne za Georgia na anagharamia $20,000 katika gharama za kuhama.
Wanandoa hao wa zamani yaani Renay na Ne-yo wana watoto watatu pamoja hivyo Ne-Yo humlipa $12,000 katika malipo ya kila mwezi ya usaidizi wa mtoto, huku pia akigharamia gharama za shule za watoto na kulipa hundi nyingine ya kila mwezi ya $3,000.
Renay aliwasilisha kesi ya talaka mnamo Agosti 2022, miezi minne tu baada ya kurejesha viapo vyao. Alidai kuwa Ne-Yo alikuwa amemdanganya “mara nyingi” na hata kuzaa mtoto kwa siri na mwanamke mwingine wakati wa ndoa yao ya miaka minane ambaye aligeuka kuwa mtoto wa kwanza wa Bagnerise.