Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuongeza muda wa safari za mabasi hayo kwa saa 24 ili Wananchi waweze kupata huduma za usafiri kwa wakati wote.
Chalamila amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa safari za magari yaendayo haraka (Mwendokasi) kutoka Gerezani hadi Mbagala ambazo zimeanza leo kuelekea msimu wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 (Sabasaba) ambapo jumla ya magari 30 yataanza kutoa huduma.
Safari hizo zinazoanza leo gharama ya nauli ni Tsh.750 kwa tiketi ambazo pia zitatolewa kwa njia ya mtandao kupitia application ya DART
Chalamila amesema “Mradi ulianza kutekelezwa kwa awamu ya kwanza, pili na tatu na imetumia fedha nyingi na zinazotolewa na Serikali na hapa ni sehemu muhimu kwani Mbagala ina Watu wengi watu wamejua kuzaa na kuongezeka na vituo vimeongezeka pia”