Ni June 29, 2023 ambapo Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group Joseph Kusaga amezungumza na Millardayo.com kuhusu ‘vision’ ama maono ya safari yake alipotoka mpaka kufikia hapa alipo leo hii.
‘Biashara ni maono sidhani kama kesho utakurupuka na kuanza biashara lazima uwe na maono, ndoto yako ni nini, umesoma sijui mpaka chuoni lakini Vision yako ni nini’-Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Vision yangu mimi toka mdogo nikiwa na miaka 17 nilikuwa na disco ya kwanza nilikuwa nawapigia Wanafunzi Mzizima pale enzi hizo nasoma Form 4 na walikuwa wanakuja wanapata burudani ikifika jioni kumi na moja wanaenda makwao’– Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Kwahiyo nikaanza Disco nikaja na Studio the first digital ilikuwa ile ambayo ilirekodi single ya kwanza ya Oyee Msela Oyee Mselaa!!, nikatoka pale nikaingia kwenye mambo ya Modeling wakina Miriam Odemba baadae nikaingia kwenye mambo ya rekodi label ambayo wakina TID, na wengine hayo yote vision yangu ilikuwa nitawale kwenye masuala ya burudani’-Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Ruge nimekutana nae miaka 22 or 23 iliyopita wakati huo ndiyo tulikuwa tunapiga disko na Ruge alikuwa wale watu wasiolala mpenda raha. Yeye alikuwa na mapenzi ya muziki na alikuwa mtoto wa kishua akija lazima umuweke pembeni umchunge ili wahuni wasimzingue’- Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Hivyo Ruge nimekua nae kwa pamoja ndani ya miaka 25 tumegombana, tumepatana tulibudu vitu mbalimbali katika sekta ya burudani kuanzia Matamasha sijui mambo ya Radio hayo yote yaliyokuwa kupigiana kile ambacho leo hii ndio kimetuheshimisha Clouds na Marehemu Ruge alikuwa ni mtu mwenye maono kifo chake kimenihuzunisha sana moyoni mwangu sitomsahau’- Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Na yale aliyoyaanza tutayaendeleza kwani Marehemu Ruge alikuwa na Upendo na kila mmoja mimi na yeye Vision zetu zilikuwa zimefanana ili kuwafungulia Dunia Vijana wa kitanzania hivyo nitaendeleza yote, Mungu ampumzike Salama na tutaendelea kumuenzi kwa yale aliyoyaanza Legancy yake iko hai’- Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Vijana wanaosikiliza haya maneno naomba uwe na Vision ama maono ndio kila kitu katika maisha ya sasa, Focus kile unachohitaji kukifanya katika biashara yako ili uweze kutimiza kile ulichokikusudia maishani’- Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
“Kujenga nchi ni kitu muhimu sana. Kwanini nchi watu wawe maskini? Hicho kitu kila siku nakataa why? Tunahakikisha tunatoa nafasi na watu wengine wanasaidia kutoa hizo ajira. Mchongo wa Kwanza wa Big Joe wa 2021 ulikuwa na mafanikio sana”- Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga
“Unaweza ukapewa Milioni 30 na zikaisha zote lakini Vision yakoni ipi jitafakari kaa fikiria nini unahitaji kufanya ambacho kitakuzalishia wewe kijana wa kitanzania amka tafakari juu ya hili Maono yako ni yapi juu ya kukomboa kile unachotaka ili kitimize malengo yako’– Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
‘Kila siku kwenye maisha unajiuliza kwanini wewe, Kwanini Mwana FA ni Mbunge, Kwanini Nikki wa Pili ni Mkuu wa Wilaya kwanini wasiwe wengine”- Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
“Hivyo Vision yangu nikuhakikisha kwamba natoa nafasi iwezekanavyo kwa vijana wengi sana wapate nafasi ya kujiendeleza katika maisha yao, kwahiyo Vijana waliojitokeza ni wengi walikuwa wanafika Elfu moja lakini nawashukuru Fauzia, Reuben kwa kufanikisha kupata vijana 55″-Joseph Kusaga
“Na sasa ka nyie Vijana mliopata ule mchongo wa Big Joe nawaomba msiwasahau Vijana wengine mkawashike mkono na kuwasaidia ili watimize ndoto zao”- Mkurugenzi Mtendaji Mkuu Clouds Media Group, Joseph Kusaga
“Nafurahi kuona kupitia #MchongowaBIGJOE kuna vijana wawili tayari ni mabilionea, walinifuata kuniuliza wanipe nini kama zawadi ya shukrani, nikawaambia wasinipe chochote, wawasaidie vijana wengine kufikia malengo yao! Mwaka huu mchongo utakuwa mchongo kubwa zaidi.” -Mkurugenzi CloudsMedia- Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga
Bado Haujachelewa hata wewe Kijana wa kitanzania itumie buku kama tiketi yako kupata Mchongo wa Big Joe.
Mchakato wa kukufikia na Kukupatia ni Wewe Kukata TIKETI kwa BUKU TU
Zawadi za MchongoPesa zinatolewa kila siku kwenye Vipindi mbalimbali vya #cloudsfm , inakuhitaji kuwa na BUKU tu .!! Ila Kujishindia hadi Mamilioni na zawadi Kibao
Hatua za kushinda zawadi hiyo na nyinginezo ni 👇
HATUA 1. Bonyeza menu yako ya malipo
HATUA 2. Chagua Lipia Bili.
HATUA 3. Kisha weka namba ya Kampuni (321333).
HATUA 4: Ingiza namba ya kumbukumbu (Andika neno PESA).
HATUA 5: Weka kiasi 1000.
HATUA 6: Ingiza namba yako ya SIRI.
HATUA 7: Bonyeza 1 KUTHIBITISHA AU 2 KUKATAA.
Ushiriki ni Miaka 18 na Zaidi, Masharti na Vigezo Kuzingatiwa.