West Ham na Arsenal bado hawajaafikiana muundo wa malipo ya uhamisho wa Declan Rice wa pauni milioni 105, ambao unachelewesha mpango mzima.
Hayo ni kwa mujibu wa gazeti la Sun, ambalo linaripoti kuwa matarajio ni kwamba maafikiano yatatimizwa lakini saa 36 baada ya makubaliano kimsingi kufikiwa bado masuala ya kutatuliwa.
Rice kwa sasa yuko likizo, kwa hivyo matibabu yoyote yatasubiri hadi wiki ijayo, lakini vilabu vyote viwili vinasalia na kazi ngumu kupata makubaliano.
Gazeti la The Sun linasema West Ham wamechelewesha mauzo ya pauni milioni 105 ya Declan Rice huku wakisubiri Arsenal kuleta mpango wa malipo unaokubalika huku West Ham wakiripotiwa kutaka kulipwa kiasi hicho kikubwa cha fedha ifikapo mapema 2025, Arsenal wanatarajia kulipa kwa nyongeza katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Mkataba huo unasemekana kukaribia kutatuliwa.
Zaidi juu ya ucheleweshaji wa dili la Arsenal kumsajili Declan Rice kuoka kwenye ripoti mbalimbali na zinasema kuwa bado hakuna makubaliano kuhusu masharti ya malipo baada ya mazungumzo ya siku mbili.
Mazungumzo bado yanaendelea.