Hapo awali Skriniar alithibitisha kuachana na klabu hiyo baada ya kukataa kusaini mkataba wa nyongeza.
Beki huyo yuko tayari kujiunga na Paris Saint-Germain kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto baada ya kukaa kwa miaka sita katika klabu hiyo ya Italia.
Beki huyo pia alitakiwa kujiunga na mabingwa hao wa Ligue 1 majira ya joto yaliyopita lakini Inter, wakati huo, ilizuia uhamisho wake kwenda mji mkuu wa Ufaransa.
Skriniar alifanyiwa upasuaji wa mgongo msimu uliopita na alikaa nje kwa muda mrefu.
Aliitwa kwenye kikosi cha Inter kwa ajili ya fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City lakini hakucheza mchezo huo.
Taarifa iliyotolewa na klabu siku ya Ijumaa ilisema, “Misimu sita iliyojaa ushindi na kuridhika: matukio ya Milan Skriniar na Inter yamefikia kikomo.
Akiwa Inter tangu msimu wa joto wa 2017, Skriniar amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika ukuaji wa ajabu wa Inter, ambayo ilianza kwa kurejea kwao Ligi ya Mabingwa mwaka 2018 na kumalizika kwa mataji matano katika misimu mitatu iliyopita.