Siku ya Alhamisi, Netflix ilitoa tangazo maalum kwa mashabiki wa Squid Game .
Jukwaa kubwa la utiririshaji wa filamu mbalimbali lilizindua waigizaji waliokuwa wakitarajiwa kuwepo kwa msimu wa pili wa mfululizo maarufu wa Korea Kusini na kufichua kuwa pamoja na waigizaji nyota wa OG, ambao ni pamoja na Lee Jung-jae, Wi Ha-joon, Gong Yoo na Lee Byung-hun, wapo watu wapya au sura mpya kadhaa ambazo pia zimejiunga na waigizaji hao.
Baada ya Netflix kutoa orodha mpya ya wasanii hao zipo taarifa ambazo badae zilikanushwa zilizo ripotiwa na Dispatch kwamba Lee Jung Jae alikuwa ameomba dhamana ya zaidi ya dola milioni 1 kwa kila episode.
Dispatch ilisema, “Netflix haiwezi kupuuza ombi la Lee Jung Jae,” na akasisitiza, “Lee Jung Jae aliuliza Netflix akitafuta dhamana kubwa ya zaidi ya dola milioni 1 kwa kila kipindi, ambayo inamaanisha kuwa ada yake ya kuonekana itafikia jumla ya zaidi ya 13. dola milioni (kwa kuzingatia vipindi 13).”
Baadae kisha shirika la Lee Jung-jae lilikanusha uvumi huo.
‘Tungependa kueleza msimamo wetu kuhusiana na ripoti kuhusu mwigizaji Lee Jung Jae kuhusika katika uigizaji wa Squid Game 2. Baadhi ya ripoti zinazodai mwigizaji Lee Jung Jae alihusika katika uigizaji wa Squid Game 2 si za kweli. Utoaji taarifa wa project zetu upo kwenye mamlaka ya mkurugenzi na kampuni ya uzalishaji, hasa, mwigizaji Lee Jung Jae anaelewa zaidi kuliko mtu yeyote kwamba kwa sababu ya kupendezwa sana na Squid Game, waigizaji wengi hufanya kazi kwa bidii ili waonekane, na [washiriki] huamuliwa kupitia ukaguzi.”