Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi amewahimiza Wanawake kushikirikiana katika jitihada za kujikwamua kiuchumi ili kujenga maisha bora kwa jamii.
Mama Mariam Mwinyi ameyasema katika mkutano wa kwanza wa Ushirikiano wa Wanawake wa China na Mataifa ya Afrika uliofanyika jana Jijini Changsha.
Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya ALL China Women Federation pia ulihutubiwa na Wake za Marais wa China, Malawi na Burundi.