Nicolas Jackson atajiunga na Chelsea kutoka Villarreal kwa €37m (£31.8m) kwa mkataba wa miaka minane baada ya kukamilisha vipimo vyake vya afya na klabu hiyo Jumapili.
Jackson alifunga mabao 12 katika mechi 26 za La Liga msimu uliopita na alikaribia kujiunga na Bournemouth Januari lakini alishindwa kufanyiwa vipimo vya afya kutokana na tatizo la misuli ya paja.
Mshambulizi huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 22 alimaliza msimu akiwa na mabao manane katika michezo mingi, akizivutia Aston Villa na Everton, lakini Chelsea wameshinda mbio za kuwania saini yake. Wamelipa zaidi ya kifungu cha kutolewa cha Jackson ili kupata masharti mazuri ya malipo ndani ya muundo wa mpango huo.
Klabu ya Chelsea na Villarreal wanasaini hati na mikataba yote hivi sasa na itakuwa takuwa rasmi hivi karibuni.
Masharti ya mkataba huo yamethibitishwa mkataba wa miaka 8, ada inayokaribia €37m kwa Villarreal lakini inalipwa kwa awamu.
Atakuwa mshambuliaji wa pili kuhamia Chelsea katika muda mfupi baada ya kuwasili kwa Christopher Nkunku kutoka RB Leipzig kwa £51m siku ya Jumanne.
Meneja mpya, Mauricio Pochettino, aliweka kipaumbele katika kuimarisha safu yake ya mbele baada ya Chelsea kuwa na wastani wa bao moja msimu uliopita na kumaliza nafasi ya 12 na kukosa kucheza soka la Ulaya.
Urefu wa kandarasi ya Jackson ni mfano wa ule unaokabidhiwa kwa wachezaji chini ya umiliki wa Todd Boehly na Clearlake Capital kama sehemu ya sera ya kutumia urejeshaji wa madeni kutumia kiasi kikubwa cha ada za uhamisho huku si kukiuka kanuni za uchezaji haki za kifedha.