Urusi yawapeleka watoto wapatao 700,000 kutoka maeneo yenye migogoro nchini Ukraine katika eneo la Urusi.
Grigory Karasin, mkuu wa kamati ya kimataifa katika Baraza la Shirikisho, baraza la juu la bunge la Urusi, alisema siku ya Jumapili.
“Katika miaka ya hivi karibuni, watoto 700,000 wamepata hifadhi kwetu, wakikimbia mashambulizi ya mabomu na makombora kutoka maeneo yenye migogoro nchini Ukraine,” Karasin aliandika kwenye chaneli yake ya ujumbe ya Telegram.
Urusi ilianzisha uvamizi kamili dhidi ya jirani yake wa magharibi mwa Ukraine mnamo Februari 2022.
Moscow inasema mpango wake wa kuwaleta watoto kutoka Ukraine katika eneo la Urusi ni kuwalinda mayatima na watoto waliotelekezwa katika eneo hilo la vita.
Hata hivyo, Ukraine inasema watoto wengi wamefukuzwa nchini kinyume cha sheria na Marekani inasema maelfu ya watoto wameondolewa kwa nguvu kutoka makwao.
Harakati nyingi za watu na watoto zilitokea katika miezi michache ya kwanza ya vita, vilivyoanza mnamo Februari 2022.
Mnamo Julai 2022, Marekani ilikadiria kuwa Urusi imewafukuza kwa lazima watoto 260,000, wakati wizara ya Ukrainia ya ujumuishaji wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu inasema watoto 19,492 wa Ukraine kwa sasa wanachukuliwa kuwa wamefukuzwa kinyume cha sheria.