Ni July 3, 2023 ambapo Mkurugenzi wa taasisi ya vijana Tanzania, Bw Gasper Paul amekutana na vyombo vya habari kuzungumza sakata la Bandari.
Taasisi hiyo imewataka watanzania Kuondoa hofu iliyopo juu ya dhamira ya Serikali kusaini mkataba baina yake na kampuni ya DP World ya Dubai wa uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa hauna kasoro zozote zinazodaiwa.
Viongozi wa Taasisi hiyo wamesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari ambao umelenga kutoa Elimu juu ya mkataba huo ambao bado Serikali haijasaini.
‘Tumewaita hapa lengo ni kuzungumza kama vijana wa Kitanzania lakini kama asasi kulizungumzia suala la DP World, kwasababu maneno yamekuwa ni mengi upotoshaji ni mkubwa kila mtu ameongea, Viongozi wa dini wamesema, Mheshimiwa Rais ameongea’- Gasper Paul
‘Sasa sisi msimamo wetu kama vijana ni kufafanua kuhusiana na mkataba huu wa DP World, kwanza mkataba haujapitishwa bado mpaka sasa Serikali ipo katika makubaliano na huo upotoshaji unaoendelea kwamba Bunge limepitisha si kweli. Vijana wenzetu wamejitokeza kuandamana kupinga wakiwa hawana fact hawajui nini kinachoendelea, hawajui chochote kwahiyo nitoe wito’- Gasper Paul