Ahmed anatuambia siri ya mafanikio yake mpaka kuaminiwa na hatimae leo hii kapewa kibali cha kuisimamia ama kuendesha kampuni.
‘Siri kubwa ni kujituma kwa kile unachokifanya asikudanganye mtu na mimi tangu naitumia hii kampuni nimekuwa mtu wa kushinda Shambani ama kuwasiliana na wafugaji ili uzalishaji uwe mwingi wa maziwa na sijabadilika mpaka nimekuwa katika ngazi ya Ukurugenzi asikuambie mtu ofisi ni shamba wala si kukaa kwenye Ma AC’- Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Ahmed Asas
‘Kingine ni Maono yako kwa kile unachokipambania mimi Familia waligundua kipawa changu mapema ndipo baadae wakaamua kunipa hii nafasi lakini siko mwenyewe bali nina wasaidizi wangu jukumu langu ni hakikisha kila kitu kinakaa katika mstari ama uzalishaji uwe mwingi’- Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Ahmed Asas
“Kuna umuhimu sana wa unywaji wa maziwa kwa watu kwani kitaalamu kwa mujibu wa Shirika la afya duniani ( WHO) wanasema binadamu anapaswa anywe maziwa walau lita 200 kwa mwaka”- Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Ahmed Asas
“Kiutaalamu wanashauri maziwa bora ni yale yaliyosindikwa na usindikaji sio kutumia kemikali,maziwa yetu yanachemshwa kuwekwa katika vifungashio vizuri na kuongezewa radha,”amesema Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Ahmed Asas
‘Hivyo mimi nahakikisha Usiku na Mchana Maziwa yanakuwa bora ndio maana hata ukifuatilia kwenye mitandao yangu ya kijamii mimi ni mtu wa kupiga sana route shambani ama labda nisafiri mahali kikazi uwa sina starehe zaidi ya hizo ndio maisha yangu ya siku zote‘- Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Ahmed Asas
‘Kwahiyo kama wewe kijana wa kitanzania ukipewa nafasi fulani ya uongozi usiichezee bali boresha mahali panapotakiwa kuwa sawa, amka piga kazi usilale hakikisha biashara inasimama na inakua’- Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Ahmed Asas
‘Na Pia ningetumia fursa hii kuwaambia Watanzania kwa ujumla kuwa tumepata nafasi kuonesha bidhaa zetu katika viwanja vya Sabasaba karibuni mtawakuta watu wetu pale Dar es Salaam watawahudumia kuhusiana na bidhaa zetu lakini pia na kuyajibu maswali mbalimbali’- Mkurugenzi wa Kampuni ya Asas Ahmed Asas