Mamlaka ya Mapato Tanzania (“TRA” au “Mamlaka”) imesema katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2022/23 (mwezi Julai 2022 hadi Juni 2023), imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 24. 11 sawa na ufanisi wa asilimia 97.4 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 24.76.
Makusanyo haya ni sawa na ongezeko la asilimia 8.2 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha 2021/22.
Aidha, katika robo ya nne ya Mwaka wa Fedha 2022/23 (mwezi April 2023 hadi Juni 2023), TRA imekusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 5.69 sawa na ufanisi wa asilimia 91.1 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 6.24, makusanya haya ni sawa na ongezeko la asilimia 1.6 ikilinganishwa na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.