Rais wa Senegal Macky Sall ameondoa wasiwasi kuwa hatokuwa mgombea wa kiti cha urais yaani muhula wa pili wa miaka mitano kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 2024 na amesema hayo katika hotuba iliyosubiriwa kwa muda mrefu kwa taifa iliyotolewa moja kwa moja kwenye Radio na Televisheni vya serikali, rais wa Senegal pia amerejelea vurugu zilizotikisa nchi hiyo..
Hali ya wasiwasi iliripotiwa kabla ya tangazo, mpinzani wake mkuu aliitisha maandamano makubwa kwa vyovyote itakavyo kuwa.
“Uamuzi wangu wa muda mrefu sio kuwa mgombea” katika uchaguzi wa urais wa Februari 25, 2024, “hata kama Katiba inanipa haki ya kufanya hivyo”, Rais Macky Sall ametangaza Jumatatu jioni.
Kinara wa Upinzani nhcini Senegal Ousmane Sonko alikuwa ameitisha maandamano zaidi kupinga uwezekano wa rais Macky Sall wa kutaka kuwania muhula wa tatu mwaka wa 2024.
Makabiliano kati ya wafuasi wa Sonko na maofisa wa polisi yametajwa kuwa mabaya zaidi kutokea nchini humo katika siku za hivi karibuni.