Culture and Development East Africa (CDEA)kwa usaidizi kutoka ubalozi wa NorwayDar-es-laam kwa kushirikiana na (TARO)Tanzania Artist Organisation wanatekeleza mradi wa miaka 3 unaokwenda kwa jina la ‘sanaa right’ ili kuimarisha mazingira ya sera na sheria kwenye tasnia ya sanaa Tanzania.
Kupitia mradi huo umeibuliwa mjadala wa Sera kuhusu hadhi ya Wasanii Tanzania, wenye lengo la kuimarisha hali na ustawi wa wasanii nchini Tanzania kupitia mageuzi ya Sera na Sheria uliofanyika jijini Dareslaaa mjadala ambao umetokana na utafiti uliofanyika wa kubaini hali ya msanii nchini Tanzania kwa kuzingatia maeneo muhimu,kamą utafiti kwenye nyanja ya elimu na mafunzo ,malipo stahiki na upatikanaji wa ufadhili ,haki za kijami na uchumi pamoja na hali ya msanii katika afya ya akili.
Sarah balozi afisa mradi sanaa right kutoka shirika la maendeleo na utamaduni CDEA amesema mradi huu umelenga kuimarisha mazingira ya sera na sheria kwa tasnia ya sanaa nchini,kutoa mapendekezo ya sera yatakayo wezesha ukuaji wa tasnia ya sanaa
‘Utafiti huo umebaini changamoto zinazo wakabili wasanii kwenye sekta mbalimbali kama ya elimu ikiwemo uhaba wa taasisi za sanaa ,uhaba wa walimu wa sanaa,elimu ya sanaa kuwa bei ghali,uwianisho kwenye wizara mbalimbali,pamoja na wasanii kuwa na ugumu wa wasanii kuaminika na kupata ufadhili ,mikopo au ruzuku na upungufu wa wawekezaji katika sanaa’.Alisema Sarah balozi afisa mradi
Aliongeza kuwa :changamoto nyingine zilizo onekana kwenye utafiti kwenye upande wa haki za kijamii ni pamoja na msanii kukosa haki za kupata mafao ya uzazi ,uzee nk.
‘Kwenye kutatua changamoto hizi kwenye sekta hizo ziongezwe taasisi za kutoa elimu ya Sanaa ,kuongezeka kwa walimu wa sanaa, lakini kwa upande wa wasanii wachukue fursa ya kuwekeza zaidi kwenye sanaa ,kusajili makampuni ya sanaa au kujiunga kwenye vyama vya wafanyakazi au mashirika ya kitaaluma ambazo zinaweza kuwawakilisha ili kuleta maslahi kwao ’ alisema
katika mdahalo wa sera uliofanyika Eco Sanaa Hub, Dar es Salaam ulahudhuriwa na watu mbalimbali ili kutoa hatua za serikali kuhusiana na sera na sheria zinazotekelekeka akiwemoDk Emmanuel Ishengoma, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Kedmon Mapana, Katibu Mtendaji, Baraza la Sanaa la Taifa – BASATA, Dk. Kiagho Kilonzo, Katibu Mtendaji, Bodi ya Filamu Tanzania na Bi Doreen Anthony Sinare, Mkurugenzi Mtendaji wa COSOTA – Ofisi ya Hakimiliki Tanzania.
Mapendekezo kadha yaliyotolewa ni wito kwa nchi walio wanachama wa UNESCO kuboresha taaluma ,hali ya kijamii na kiuchumi ya wasanii,kupitia utekelezaji wa sera na hatua zinazohusiana na mafunzo ,usalama wa kijamii ,ajira, mapato na masharti ya kodi na uhuru wa kujieleza.