Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni ametoa onyo kwa Taasisi za Dini ambazo zimekua zikitoa mahubiri kinyume na Mila na Desturi za Mtanzania.
Akiongea na Waandishi baada ya Mkutano wake na Viongozi wa Dini amesema hawatasita kuchukua hatua kwa Taaisisi zenye chokochoko.
Alipoulizwa kuhusu Video ya Zumaridi inayosambaa Mtandaoni ikimuonyesha Mhubiri huyo akiwaambia Watoto yeye ni MUNGU
“Kuna taasisi ambazo zimekuwa zikiibuka wala hazijaja kusajiliwa kama hiyo unayozungumza hajasajiliwa ni mtu katoka tu hiko anasema Yeye ni Kiongozi wa Dini mwingine anahamasisha mambo ya jinsia moja, mwingine anajiita MUNGU”
“Serikali haiwezi kukubali imekuwa ikichukua hatua kwa Taaisisi au watu wa namna kama hiyo wanaofanya vitendo kinyume na mila na desturi”
“Mtu yoyote atachukuliwa hatua” Masauni