Kama ulikuja Dar es Salaam miaka kumi iliyopita na ukirudi kwasasa basi lazima ukute mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika Sekta mbalimbali kuanzia Barabara, Majengo na mengineyo.
Ukiacha uboreshwaji uliofanywa kwenye sekta mbalimbali kingine ambacho kimenivutia ambacho huenda utapendezwa nacho.
Ni Kwamba Tips wamefanya mapinduzi makubwa na kutoa ajira katika sekta ya viota vinavyowakutanisha watu mbalimbali ukiacha ile Tips Mikocheni aliyoifungua Mwaka 2017 sasa kwa Mwaka 2022 walitumia Fursa na kufungua chimbo lingine lenye utofauti liitwalo Tips Coco Beach lililopo Oysterbay Dar es Salaam.
Tips wanastahili pongezi na wameweza kuwa wa kitofauti na maeneo mengine ya Dar kwa huduma zao pamoja kwa ubunifu walioufanya wa kuamua kuiteka Jumatatu ambayo wengi tumezoea ni siku ya kazi lakini wao wamekuja na kitu cha tofauti.
Hizi ni baadhi ya picha ushuhudie kile kilichojiri Jana Julai 3, 2023 ambapo shangwe lilikuwa si la kitoto, tazama picha hizi hakika Dar es Salaam kama mamtoni Partie After Partie.