Kocha wa Real Madrid Muitaliano Carlo Ancelotti atachukua nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya Copa America 2024, chanzo kutoka Shirikisho la Soka la Brazil kiliiambia AFP Jumanne.
Shirikisho hilo lilikuwa limetangaza hapo awali kwamba Fernando Diniz wa Fluminense angeiongoza timu hiyo katika kipindi cha mpito.
Ancelotti amesalia na msimu katika mkataba wake na Real na atachukua mikoba ya Brazil kwa wakati kwa Copa America itakayofanyika Marekani kuanzia Juni 2024.
Ancelotti, 64, atakuwa kocha wa timu ya taifa kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya ukocha, akichukua nafasi ya Tite, ambaye aliondoka kwenye nafasi hiyo baada ya kushindwa katika robo fainali na Croatia kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar.
Kocha huyo wa zamani wa AC Milan na Chelsea atakuwa mgeni wa kwanza kuifundisha Brazil katika takriban miaka sitini.
Kocha wa mwisho wa kigeni wa Brazil alikuwa Muajentina Filpo Nunez ambaye aliongoza kwa mchezo mmoja mnamo 1965.
Miongoni mwa mafanikio yake mengi, Ancelotti mwenye umri wa miaka 64 ameshinda Ligi ya Mabingwa mara mbili akiwa na AC Milan na Real Madrid.
Pia ameshinda mataji ya ligi ya nyumbani nchini Uingereza akiwa na Chelsea, Ujerumani akiwa na Bayern Munich na Ufaransa akiwa na Paris Saint-Germain pamoja na Real na Milan.
Brazil walifundishwa na Tite kwenye Kombe la Dunia mwaka jana, lakini alishuka kwenye nafasi hiyo baada ya kuondolewa katika hatua ya robo fainali dhidi ya Croatia.