Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ramadhan Mlao anatarajia kufanya mkutano wa kichama katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Millardayo.com Bw. Ramadhani Mlao alisema Mkutano huo utafanyika katika Chuo cha Duce kilichopo Wilayani humo.
‘Viva CCM Viva, Viva Mama Samia Viva, Kwanza kabisa ningechukua nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake wenye tija kwa taifa hili pamoja na wasaidizi wake kwani Serikali hii ni Serikali yenye kusikiliza Wananchi wake’- Ramadhan Mlao
‘Kwa Mfano Juzi tu tumemsikia Naibu Waziri wa Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Injinia Kundo Mathew amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la Wizara hiyo chini ya Waziri Nape Moses Nnauye la kufuta tozo katika miamala ya simu na hatimae yametimia kuwa Mama yetu Samia ameruhusu na kutoa maelekezo tozo inayotokana na miamala ya simu iondolewe, hakutokuwa na tozo kwenye miamala ya simu, ile tozo mliokuwa mnasema Rais ameshapangua huyu ndio Mwanamapinduzi halisi wa maendeleo ya Taifa letu’ – Ramadhan Mlao
‘Hongera kwa Rais wetu na Hongera kwa Wasaidizi wake na la mwisho kumalizia hapa ambalo ni la msingi Mnamo Julai 8, 2023 nitakuwa na Mkutano wa kichama ambao ni Semina ya Darasa la itikadi Wilayani Temeke katika chuo cha Duce sitokuwa pekee yangu pia nitakuwa na Viongozi mbalimbali wa Chama karibuni tuijenga UVCCM karibuni tuijenga CCM karibuni kwani haya ndio maendeleo Chanya yatakayonufaisha vizazi vyetu vya baadae karibu mjifunze mengi’- Ramadhan Mlao