Mkuu wa Moa wa Shinyanga Christina Solomon Mndeme amezitaka Taasisi za Dini kuendelea kukemea vitendo vyote visivyo na Maadilu ya Kitanzani , amesema hayo leo tarehe 6 Julai, 2023 wakati aliposhiriki katika maadhimisho ya upadirisho wa Shemasi James Furaha Mrema sherehe zilizofanyika katika Parokia ya Msalaba Mtakatifu – Mwadui hapa Mkoani Shinyanga.
Katika sherehe hizi ambazo zimeongozwa na Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo kuu Katoriki, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali.
Pamoja na maelekezo mengine lakini Mhe. Mndeme amezitaka Taasisi za Dini kuendelea kukemea na kudhibiti kabisa vitendo vyote visivyo na maadili, utu wala mila zetu za kitanzania.