Mbunge Viti Maalum kundi la Walemavu Khadija Shaaban maarufu Keisha amesema Serikali imetoa kiasi cha fedha Bilioni 3.4, kwa lengo la kukarabati Vyuo vyenye mazingira rafiki kwa Watu wenye ulemavu mikoa ya Dar es salaam, Mtwara, Tanga na Tabora.
Keisha amezungumza hayo Jijini Mwanza alipokutana na Watu wenye ulemavu kusikiliza matatizo wanayokumbana nayo kwenye jamii wanazoishi na kuahidi kuziwasilisha Bungeni ili zitafutiwe ufumbuzi.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza Amos Makalla amekemea vikali tabia inayofanywa na baadhi ya vyombo vya Usafiri ya kuwabagua na kuwabeza Watu wenye ulemavu na kuiagiza Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwachukulia hatua wote watakaobainika kuwanyanyapaa watu hao.