Ni msanii wa nyimbo za Asili, Mrisho Mpoto ambae leo amefika katika Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Miongoni aliyoyazungumza ni kuhusiana na leo ikiwa siku muhimu ya kuadhimisha siku ya Kiswahili Duniani.
‘Tarehe 7 mwezi wa 7 ni maadhimisho Ya siku ya KISWAHILI Duniani na kama utakumbuka Mwaka Jana mimi na timu yangu tulipata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika maadhimisho haya ambayo yalifanyika rasmi nchini Ufaransa’- Mrisho Mpoto
‘Na Serikali iliniamini na kutambua kupitia nyimbozangu hizi za Asili kuwa naweza kukitangaza Lugha yetu ya Kiswahili ndio Uzalendo wenyewe’- Mrisho Mpoto
‘Kwahiyo nichukue Fursa hii ya kipekee kuwataka Watanzania wote kwa ujumla mjivunie lugha hii kwani ndio utambulisho wako wewe na taifa lako tukithamini Kiswahili kama Mataifa mengine wanavyothamini lugha zao hata Marehemu hayati Magufuli alisema tujali Utanzania na tusidharau kile tulichobariki’- Mrisho Mpoto
Hizi ni baadhi ya picha zikimuonesha Mrisho Mpoto akiwa katika banda la Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.