Klabu ya Paris Saint-Germain wanaamini Kylian Mbappe tayari amekubali kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure msimu ujao wa joto.
Mbappe aliandikiwa barua na PSG Jumatatu ikiweka wazi kuwa atauzwa msimu huu wa joto isipokuwa atakubali kuongeza mkataba wake kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Siku za nyuma ilidhaniwa kuwa PSG ingependelea kutofanya biashara na Real Madrid, lakini Mbappe asipoongeza mkataba, watamuuza kwa yeyote ambaye anaweza kumudu kumnunua.
Lakini sasa Kylian Mbappe amepewa tarehe ya mwisho ya Julai 31 kujitolea kusalia PSG hadi angalau msimu wa joto wa 2025, vinginevyo atauzwa kwa dau kubwa zaidi mwezi ujao; Mkataba wa fowadi wa Ufaransa unakamilika 2024 lakini PSG walikuwa wakimtarajia kutumia chaguo la kuongeza muda kwa miezi 12.
Bei inayoulizwa kumpata mbappe inaweza kuwa takriban £150m.
Jumatano, akizungumza baada ya kumtambulisha Luis Enrique kama meneja mpya wa klabu hiyo, Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi alisema: “Msimamo wangu uko wazi sana. Sitaki kurudia kila mara: ikiwa Kylian anataka kubaki, tunataka abaki. Lakini anahitaji kusaini mkataba mpya.
“Hatutaki kumpoteza mchezaji bora wa dunia bure. Hatuwezi kufanya hivyo. Hii ni klabu ya Ufaransa.
“Alisema hataondoka bure. Ikiwa atabadilisha mawazo yake leo, sio kosa langu. Hatutaki kumpoteza mchezaji bora wa dunia bure, hilo liko wazi.”
Katika barua ya Jumatatu, PSG ilimwambia Mbappe uamuzi wake wa kutoongeza mkataba umeisababishia klabu madhara makubwa.