Waziri wa madini Dotto Biteko amefanya ziara katika ukuta wa madini ya Tanzanite mirerani Mkoani Manyara ambapo wakati akiongea na watumishi,Luten clemence akimuwakilisha date kamanda amesema kuwa wakati wakiendelea na ukaguzi walimkamata mtu mmoja kwenye chumba cha upekuzi akitaka kutorosha madini.
Waziri wa madini Doto Biteko amesema hawajazuia uuzaji wa madini ndani ya ukuta bali wanachokipinga ni utoroshaji wa madini na kwamba serikali imejipanga kurudisha minada ya madini kwa ajili ya kutangaza Tanzanite ijulikane duniani.