Uongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Temeke umefanya Semina maalumu kwa Viongozi wa UVCCM Jimbo la Temeke iliyohusisha Viongozi wa Matawi na Kata za Jimbo hilo Mafunzo hayo ya Uongozi na Itikadi ya Chama Cha Mapinduzi yalihudhuriwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia kundi la Vijana Ndg.Ramadhan Mlao (MNEC) alikuwa mgeni rasmi wa Semina hiyo.
Pamoja ya Semina hiyo Ndg. Ramadhan Mlao (MNEC) aliweza kupata Wasaa wa Kuzindua Mashina Mawili katika Tawi la KEKO JUU Kwa kuzindua Mawe ya Msingi na Kupandisha Bendera za CCM kwenye Mashina hayo. Uzinduzi huo uliambatana na matembezi ya Vikundi mbalimbali ikiwemo bodaboda, Mafundi Seremala, na Vijana wa CCM waliombatana na Jopo la Viongozi lililoongozwa na Ndg. Mlao (MNEC) mgeni Rasmi, Ndg. Nasra Mohamed (M/Kiti UVCCM (M) DSM) pamoja na Viongozi mbalimbali.
Aidha, Kupitia Semina hiyo Ndg.Mlao aliwaasa Vijana wa CCM kuwa kitu kimoja kukisaidia Chama Cha Mapinduzi kwa kuimarisha mahusiano mazuri miongoni mwa Vijana kwa kudumisha Umoja, Upendo na Mshikamano na kuacha tabia za Chuki na Ubinafsi ambazo kimsingi hazina Afya kwa Ustawi wa Chama chetu na kuwatazamisha Vijana kuwa Wana kazi kubwa ya Kufanya kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Jamii inafahamu kazi kubwa inayofanya na Chama chetu kupitia Serikali hii ya Awamu ya Sita.
Pia, alitoa pongezi kwa Uongozi wa UVCCM Mkoa wa Dar es salaam kwa kazi kubwa Wanayofanya ya kuimarisha Jumuiya ya Umoja wa Vijana, kuisemea Serikali katika Utekelezaji wa miradi na kuongezea kwa kusema Dar es salaam kazi inaendelea kwa weredi na kasi kubwa, kisha akawashukuru Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Temeke kwa Mapokezi mazuri na Kuandaa jambo lenye tija kwa kuwaongezea maarifa hasa katika maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 akawaagiza Viongozi mafunzo haya yawe endelevu ili kujenga Makada mahiri kwa Chama chetu.