Kijiji cha nyuki company limited kinachojiusisha na maswala ya ufugaji nyuki, Ulinaji na uuzaji wa Asali, kilichopo Mkoani Singida siku ya jana katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jiijni Dar es Salaam wameelza nnamna ya ufugaji nyuki.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa kijiji cha nyuki company limited Philemon Josephat amesema kuwa..‘Kijiji cha nyuki ni eneo la ukubwa wa ekali 5000 ambalo lipo katika mkoa wa Singida, ambapo kinajiusisha na ufugaji wa nyuki, uzalishaji na usambazaji wa Asali, kwa miaka kumi na mbili iliyopita kijiji hiko kimekuwa na wafanyakazi takribani 167 ambao wanashiriki katika zoezi la kusambaza maarifa ya nyuki nchini kupitia kijiji cha nyuki open school’