Harry Maguire kwa sasa anafanya mazoezi makali nchini Ureno ili kurudisha imani ya Erik ten Hag katika kikosi cha Manchester United.
inasemekana kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza anafanya mazoezi mara tatu kwa siku nchini Ureno pamoja na mlinzi wa zamani wa Ureno na Chelsea, Ricardo Carvalho katika jitihada za kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha Erik ten Hag huko United, kulingana na Fabrizio Romano.
Licha ya kuwa nahodha wa klabu, Maguire alipoteza nafasi yake ya mwanzo ya United msimu uliopita baada ya kuwasili kwa Lisandro Martinez .
Alionekana kwenye Premier League mara 16 pekee na alitumia dakika 759 uwanjani.
Kwenye taarifa nyepesi nyepesi beki huyo amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka United msimu huu wa joto huku klabu kama Tottenham, West Ham na Newcastle zikionyesha nia ya kutaka kumsajili.