Zaidi ya wiki moja iliyopita, Lil Uzi Vert alitoa albamu yake ya “Pink Tape” iliyokuwa ikitarajiwa yenye nyimbo 26 mpya pia zilitolewa, zikiwemo alizowashirikisha mastaa wakali kama Nicki Minaj, Travis Scott, Don Toliver, na zaidi.
Kwa sababu hiyo, Pink Tape imetoka kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard 200, na pia kumpa Uzi nafasi kubwa zaidi ya wasikilizaji wa ngoma zake Spotify,na ni zaidi ya streamers milioni 60 na zaidi ya hayo, pia ni albamu ya kwanza nambari moja kufikia mahali hapo, mnamo 2023.
Wakati huo huo, Uzi pia amekuwa akidokeza kuhusu sehemu ya tatu ya mfululizo wake wa “Luv Is Rage”.
Wiki iliyopita, alidokeza inakuja hivi karibuni, kwa kuweka “Luv Is Rage 3” kwenye page yake ya Instagram.
Hii ni karibu miaka sita baada ya muendelezo huo kutolewa. Sasa, rapper Philly anafafanua ni lini mashabiki wanaweza kutarajia project hiyo kuwasili.
Shabiki mmoja alimuuliza Uzi lini Luv Is Rage 3 inakuja, huku akitania wazo la kuitoa baada ya “miezi michache.”
Huku mashabiki wakisubiri Luv Is Rage 3, Uzi pia atakuwa na Ziara yake ya “Pink Tape”, msimu huu wa kiangazi na itaanza Oktoba 24 huko Minneapolis, MN, na kuhitimishwa mnamo Novemba 22, katika mji alipotokea lil Uzi vert wa Philadelphia.