Iran itashuhudia kurejea kwa watazamaji wa kike katika viwanja vya michezo ya ligi kuu mwaka huu, bosi wa soka nchini humo alisema, na kuashiria ushindi mkubwa kwa wanawake dhidi ya marufuku ya muda mrefu ya kuhudhuria mechi za soka.
Nchi hiyo iliwazuia kwa kiasi kikubwa wanawake kuzuru viwanja vya michezo kwa ajili ya soka na mechi nyinginezo tangu mapinduzi ya Kiislamu ya 1979, licha ya kuwa hakuna sheria inayowakataza kuingia.
“Mwaka huu, moja ya sifa kuu za ligi hii…ni kwamba tutashuhudia kuingia kwa wanawake viwanjani,” mkuu wa Shirikisho la Soka la Iran Mehdi Taj alisema.
Tangazo hilo lilikuja katika hafla ya kuchora kwa msimu wa kandanda wa Iran, unaojumuisha timu 16, ambayo imepangwa kufanyika mwezi ujao.
Viongozi wa dini nchini Iran, ambao wana jukumu kubwa katika kufanya maamuzi kwa ajili ya nchi, wamesema kwamba wanawake lazima walindwe dhidi ya hali ya uanaume .
Hata hivyo, pamoja na hayo yote, Taj siku ya Jumapili ilithibitisha kwamba baadhi ya viwanja vya michezo katika miji ya Isfahan, Kerman na Ahvaz – lakini si mji mkuu Tehran – vilikuwa “tayari” kuwakaribisha wanawake.
Mnamo Agosti, wakati klabu ya Tehran Esteghlal ilipocheza na klabu nyingine, Mes Kerman, wanawake waliruhusiwa kwa mara ya kwanza kuhudhuria mechi ya soka.
Katika tukio lingine, takriban wanawake 4000 waliruhusiwa kuhudhuria mechi ya Irani ya Kufuzu Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Kambodia kwenye Uwanja wa Tehran Azadi mnamo 2019.
Iran imekabiliwa na shinikizo kubwa kuwaruhusu wanawake kuhudhuria mechi baada ya kifo cha ya shabiki wa kandanda Sahar Khodayari, ambaye mwaka wa 2019 alijichoma moto kwa kuhofia kufungwa jela alipokuwa akijaribu kuhudhuria mpira wa miguu nakujifanya kama mwanamume.