Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amekagua ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere, (JNHPP) na kuona kazi zinavyoendelea kufanyika hadi usiku.
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imebainisha kuwa mpaka kufikia mwezi Juni 2024, Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) litaanza kutoa huduma ya uzalishaji wa umeme.
Alisema mradi huo una faida nyingi ikiwa ni pamoja kilimo kwani mahitaji ya umeme yameongezeka kwa kasi katika mwaka huu unaoisha, ambapo rekodi ya kiwango cha juu cha mahitaji ya umeme (peak demand), jambo ambalo siyo la kawaida katika historia ya mahitaji ya umeme nchini
Waziri wa Nishati, January Makamba (kushoto), akisikiliza maelezo katika eneo inapojengwa mitambo ya kuzalisha umeme katika Mradi Wa Umeme wa Julius Nyerere kulia akiwa nimhandisi mkazi TECU
Waziri pia wakati wa kukagua mradi huo amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo wa kihistoria, Taifa litakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya Megawati 2115, kiasi ambacho ni kikubwa cha umeme ambacho kinatarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya nishati mijini, vijijini na nchi jirani.
Waziri wa Nishati, January Makamba akiendelea kutembelea na kukagua eneo la mradi wa kufua umeme akijionea tuta kuu,power water ways,power house pamoja na switchyard.
Waziri wa Nishati, January Makamba akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kidini ambao pia ni wageni kwenye ziara hiyo pamoja na viongozi wa TEC na CCT
Waziri wa Nishati, January Makamba , akiangalia kazi mbalimbali zinazoendelea kufanyika katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere akiwa na Mhandisi Mkazi wa Mradi, na wageni wengine walipotembelea Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere.
Maeneo waliyokagua ni pamoja Tuta Kuu la Bwawa, njia za kupeleka maji kwenye mitambo ya kuzalisha umeme, Jengo la mitambo pamoja, kituo cha kupokea na kusafirisha umeme.
Mwelekeo wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 ni nchi yetu kuwa Taifa la viwanda, lenye uchumi wa kati na lenye bidhaa na huduma zinazoweza kushindana katika masoko ya kikanda na kimataifa. Kwa kuwa viwanda vinahitaji nishati ya uhakika na gharama nafuu, kufikiwa kwa azma hii kunahitaji uwekezaji madhubuti katika mnyororo mzima wa uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa nishati katika maeneo ya uzalishaji.
Azma ya Wizara ni kuhakikisha wananchi wote nchini wanafikiwa na huduma ya umeme, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Vitongoji vyote vinapata umeme ndani ya muda mfupi, badala ya wananchi wa maeneo hayo, wenye kiu kubwa ya nishati hiyo kusubiri kwa takribani miaka 20 kwa utaratibu wa sasa wa upelekaji umeme katika Vitongojini na hivyo kuwacheleweshea maendeleo na kuendelea kuwanyima fursa na manufaa yatokanayo na nishati hiyo.