Headlines za dunia pia zimegonga sana kwenye siku hizi za karibuni kuhusu mwanamke wa Sudan ambae amekua akisubiria hukumu ya kunyongwa kwa kosa la kuolewa na mume mkristo huku dini ya baba yake ikiwa inajulikana wazi kwamba ni Muislamu.
Wizara ya mambo ya nje nchini Sudan imesema kuna uwezekano wa Meriam kuachiwa huru ndani ya siku kadhaa zijazo hivyo hukumu ya kifo inayomkabili inaweza isiwepo manake Sudan ni nchi inayoheshimu uhuru wa watu kuabudu.
Hukumu hiyo aliipata baada ya kugoma kubadili dini na kurudi kwenye Uislamu ambao ni dini ya baba huku mama yake aliemlea akiwa ni Mkristo.
Meriam ambae yuko kwenye ndoa na Daniel Wani tangu mwaka 2011, alijifungua mtoto wake wa pili akiwa gerezani Jumatano iliyopita ambapo vyombo vinne vya habari vya kimataifa vimeripoti kwamba alijifungua akiwa bado na minyororo
Wakili wa Ibrahim pamoja na mumewe Daniel wamesema hawajafahamishwa chochote kuhusiana na mipango ya kumwachilia huru.
Mahakama ilisema Meriam angeweza kumuhudumia mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu yake kutekelezwa ambapo taarifa nyingine ya juzi ilisema Mwanaume huyu amepewa ruhusa ya dakika ishirini kila wiki kwenda kumuona mke wake gerezani.
Unaambiwa nchi ya Sudan ina idadi kubwa ya Waislam na sheria za kiislamu zimekuwa zikipewa uzito tangu mwaka 1980.