Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)hii Leo wametembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere, kwa lengo la kuona hatua iliyofikiwa utekelezaji wa mradi huo, ambao kwa sasa umefikia asilimia 90.
Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo unaojengwa katika Bonde la mto Rufiji waziri wa nishati mh january makamba aliyeambatana na viongozi hao kwenye ziara hiyo alipongeza kasi ya ujenzi wake na kubainisha kwamba hivi sasa ujazo wa maji ndani ya bwawa umefikia mita 163.7 kutoka mita 193 kutoka usawa wa bahari kiasi ambacho ni kikubwa ambacho kinatarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya nishati
“Kama mnavyofahamu kuwa mradi huu una maisha na katika maisha yake kuna alama, vituo mbalimbali ambavyo vinafikiwa kwa vipindi ambavyo ni muhimu, sasa hivi tumefikia kwenye mafanikio makubwa kuliko yote tangu tuanze ujenzi na yenyewe ni kujaza maji kwenye bwawa,” alisema.
Waziri huyo ameongeza kwa matarajio ya mardi huo ni kuanza kwa majaribio kuzungusha mitambo hiyo kwa nguvu ya maji mwezi 2 mwakani kisha mwezi juni, mwaka ujao kuanza kuingiza umeme katika gridi ya taifa.
Mradi huo unatarajiwa kuzalisha megawati 2,115 zitakazoongeza nguvu katika megawati 1,500 zinazozalishwa na vyanzo mbalimbali vya sasa na kuondoa tatizo la uhaba wa umeme nchini huku ongezeko hilo la megawati 2,115 likiwezesha Tanzania kujitosheleza kwa mahitaji yake ya umeme na kuwa na ziada ya kuuzwa nchi jirani sambamba na kupunguza gharama za umeme kwa Watanzania.