Story zilizopamba moto kwenye cahat za mashabiki wa mchezaji nyota wa Manchester City Erling Haaland baada ya kuonekana kwenye picha ya pamoja na mwanamitindo maarufu Kim Kardashian katika hafla ya Dolce & Gabbana yaendelea kutengeneza sura mpya .
Ingawa inaweza kuonekana kuwa hakuna uhusiano kati ya mshambuliaji huyo wa Norway na mtu mashuhuri wa mtindo wa maisha, wawili hao ni mabalozi wa chapa maarufu ya mavazi, Dolce & Gabbana.
Gumzo lilianza pale ambapo nyota huyo wa Marekani alichapisha picha nyingi kwenye Instagram yake ikiwa ni pamoja na picha hiyo akiwa na Haaland.
Mashabiki mara moja walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha hiyo kufichua kuhusu Kardashian kuungana na Kylian Mbappe wa PSG wiki moja iliyopita je kuna nini kati ya Kim na wachezaji hao.lakini hakuna majibu kati yao wote wawili zaidi ya brand ambassador wa chapa hiyo maarufu.
Haaland bado ana mudawa mapumziko mwake kabla ya Premier League kuanza mazoezi na Manchester City.
Raia huyo wa Norway aliongezewa siku za mapumziko kwani alihusika katika mechi za kimataifa mwishoni mwa msimu uliopita.